click here

click here

Pongezi za Lowassa kwa Rais Magufuli

Pongezi za Lowassa kwa Rais Magufuli

Aliyekuwa Waziri Mkuu ambaye kwa sasa ni  mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mh. Edward Lowassa ametoa rai kwa watanzania kumuacha Rais Dkt. Magufuli kuendelea kupitisha fagio sehemu mbalimbali kwani nchi ilipokuwa imefikia ni pabaya.
Lowassa amesema kuwa ni kweli kuna baadhi ya mambo anakosea lakini si wakati wake kumkosoa kwa sasa, hivyo watanzania wanatakiwa wamuunge mkono kwa kile anachokifanya kwakuwa anafanya kwa maslahi ya Taifa.
“Rais Magufuli ameanza vizuri kwa kubana baadhi ya mambo ambayo hayakuwa ya msingi, kuna mambo mazuri sana mengi ameyafanya mapaka dakika hii, lakini mwalimu Nyerere alishawahi kusema kuwa wakati unafagia ni lazima uwe makini kwani unaweza kufagia hata shilingi, na sasa Rais Magufuli anafagia shilingi nyingi, kwasasa tumuache afanye kazi yake lakini tutamhukumu muda ukifika,”amesema Lowassa.

No comments

Powered by Blogger.