Home
>
makala
>
STORYGRAM1: Fahamu jinsi Damu ya Hedhi ya Mwanamke Ilivyo na Nguvu Katika Imani za Kishirikina.
STORYGRAM1: Fahamu jinsi Damu ya Hedhi ya Mwanamke Ilivyo na Nguvu Katika Imani za Kishirikina.
Fahamu jinsi Damu ya Hedhi ya Mwanamke Ilivyo na Nguvu Katika Imani za Kishirikina.

Nitangulie kuomba radhi kwa wale watakaokereka na hii mada..Nina heshima
kubwa kwa akina mama wote na privacy yao..naomba tuichukulie hii kwa
muktadha wa maarifa, elimu na ufunuo wa dunia ya upande wa imani
Makuzi yetu yametulea kutufundisha kwamba damu husika ni uchafu na jambo
la Siri sana... Wahusika kwenye hili hufanya ni jambo la siri huku
wengine wakijichukia kabisa
Kwa dhima ya udugu wa kishetani damu ya hedhi ni kitu cha thamani kubwa
kwakuwa imebeba uhai nguvu na kiwakilishi cha maisha marefu, ikijulikana
kama nyota ya moto kiashiria cha mungu mwezi...kwenye ibada za
kishetani alama nyekundu ni kiwakilishi cha hiyo damu na hata wale
ANNUNAKI(malaika walioanguka) wanaichukulia kama dhahabu ya miungu kwa
imani yao
Hedhi mzunguko wake unatawaliwa na mizunguko ya mwezi na kuna mahusiano
ya moja kwa moja kati ya damu ya hedhi mzunguko wa mwezi na mwanamke!
Kwa wenzetu wahindi hii wanaita SOMA na Greece ikijulikana kama AMBROSIA...Tafsiri kwa muktadha wao ikiwa asali ya miungu. ...
Mwezi ni alama ya makazi ya mungu na malaika wa kike. Hivyo basi ibada
yoyote inayouhusika na kunywa damu ya hedhi, hiyo ni ibada ya kuabudu
mwezi kwa maana ya kumuabudu mwanamke
Hapa kuna mifakarano kwa baadhi ya wayahudi kwakuwa baadhi yao hupenda
kufuata kalenda ya mwezi na hata miungu yao mingi ikiwa ni masanamu ya
kike lakini wale wanaojiita Israeties wakipinga hilo kwakuwa wanaamini
anayepaswa kuabudiwa ni mungu jua hivyo kuabudu mwezi ni kuruhusu
kutawaliwa na mwanamke....
Tukiachana na hao hapa kwetu damu ya hedhi hutumika kutengeneza dawa za
mvuto wa kimapenzi na ishu za kishirikina kufarakanisha ama hata
kupatanisha...!
Vyovyote iwavyo hiki tunachodhani ni uchafu kina siri yenye nguvu kubwa kwenye ulimwengu wa roho
chanzo udakuspecially
Post a Comment