click here

click here

Pauni Milioni 165 kiganjani kwa Wenger, Aambiwa Msimu Ujao Ubingwa Utue Emirates Stadium.

Pauni Milioni 165 kiganjani kwa Wenger, Aambiwa Msimu Ujao Ubingwa Utue Emirates Stadium.

Kocha wa Arsenal ajulikanaye kama  Arsene Wenger mwenye sifa ya ubahili, amekabidhiwa kiasi kikubwa cha fedha huku akitakwa  zitumike kufanya usajili wa wachezaji wapya.
Wamiliki wa klabu hiyo wamemtengea kocha huyo Mfaransa Pauni 165 milioni na kumweleza azitumie kuimarisha kikosi chake.
Lengo la wamiliki hao kumpatia fedha hizo Wenger ni kushindana na wababe wengine England kwenye soko la usajili.
Tayari, Wenger anayo majina ya Riyad Mahrez wa Leicester City na Mturuki Arda Turan ambaye ameachwa na Barcelona.
Wenger ameambiwa awe makini na kikosi chake Arsenal msimu ujao kwani mwisho wa msimu atatakiwa kutwaa taji ambalo amelikosa tangu msimu wa 2004.

No comments

Powered by Blogger.