Picha ya busu la Beckham kwa binti yake Nchini lazua gumzo.
Picha ya busu la Beckham kwa binti yake Nchini lazua gumzo.

Mkali wa soka, David Beckham aliyetua nchini
Tanzania hivi karibuni, ameibua maneno kwa wazazi kufuatia kitendo chake cha kuweka picha itandaoni inayomuonesha akimbusu mwanaye mdomoni.
Baadhi ya wazazi walifunguka kwa kusema kuwa picha hiyo haina maadili na inaleta fikra mbaya
ukizingatia mwanae Harper ndio kwanza ana umri wa miaka mitano
tu.
“Kwa kuwa mkweli, kumbusu mwanao wa kike mdomoni kama hivi kidogo inashangaza… ndio inashangaza,” aliandika mtu mmoja.
“Ninajaribu kutohukumu lakini nashindwa, lakini nadhani kidogo
inashangaza na sio sawa kuona anambusu mwanae kwenye midomo kwa
kuzingatia umri wake,” aliandika mwingine.
Hata hivyo, wazazi wenye mtazamo tofauti walijitokeza kumtetea mwanasoka huyo ambaye ni baba wa watoto wanne.
“Ni picha nzuri ya upendo inayoonesha uhusiano mzuri kati yako (Beckham) na binti yako,”
aliandika shabiki mmoja. “Achana na wenye chuki. Ni wapumbavu. Harper
sio binti mdogo, ni mtoto mdogo tu na hakuna ubaya kwa hilo,” aliandika
mwingine.
Hivi karibuni, Beckham alionekana akiingia Tanzania kwa ajili ya
kutembelea mbuga za wanyama, akiwa na familia yake. Ujio huo ulionekana
kuwa binafsi na wa kimyakimya.
Post a Comment