Kichwa Bandia cha Trump chamtia matatani Mchekeshaji.
Kichwa Bandia cha Trump chamtia matatani Mchekeshaji Cathy Griffin.
Mwanamama Cathy Griffin ambaye ni msanii mchekeshaji raia wa Marekani alieonekana mubashara kupitia kipindi cha TV kinachorushwa na CNN akiwa ameshika kinyago
kinachofanana kabisa na kichwa cha Rais Donald Trump, huenda akashtakiwa
kutokana na kile kilichotajwa kama kuvuka mipaka ya Uhuru wa Habari.
Mwanamama huyo mwenye umri wa miaka 57 alionekana akiwa amebeba kinyago cha
Rais Trump akiwa amekatwa kichwa, Jambo ambalo limezua hasira miongoni
mwa raia wa Marekani pamoja na Rais Trump.
Msanii huyo alifukuzwa kazi maramoja na Kituo cha TV cha CNN ambacho kilitangaza kufuta kipindi chake kuruka hewani.
Baadhi ya watu maarufu nchini Marekani akiwemo Rais Trump mwenyewe
wamekilaani kitendo hicho na kusema ni dhihaka na udhalilishaji kwa
familia za Wanajeshi na baadhi ya waandishi wa habari wa Marekani
waliochinjwa na Kikundi cha kigaidi cha ISIS.

Post a Comment