Ni siku kadhaa sasa zimepita tokea siku ambayo wakali na mastaa wa filamu za Kibongo, Chuchu Hans na
Vincent Kigosi ‘Ray’ kupanga kufanya shughuli ya kumtoa Jaden nje maarufu kama 40,kudaiwa kubuma,
mwanamama huyo amefunguka kuwa licha ya kuchelewa bado ipo na inakuja
‘soon’. Chuchu aliongea hayo baada ya habari kuenea kuwa mastaa hao
wameshindwa kumfanyia mtoto wao sherehe ya kumtoa nje ‘40’ kutokana na
hali ya kifedha kuwa mbaya kwao.
“Ni kweli tumechelewa kumfanyia 40 mtoto wetu lakini ‘soon’ itafanyika
tu na haya yote yanatokana na maamuzi ya baba yake ndiye aliyepanga
hivyo siyo kukosa pesa kama wanavyodai, siku ya shughuli ikikaribia
utasikia fununu tu,” alisema Chuchu.
Post a Comment