storygram1: Mghwira "Mimi siyo mpinzani wa maendeleo nimepewa jukumu la kutekeleza maendeleo ya nchi,"
Mghwira "Mimi siyo mpinzani wa maendeleo nimepewa jukumu la kutekeleza maendeleo ya nchi,"
Aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalen Anna Mghwira ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, mesema kuwa uamuzi wa kumvua
uenyekiti uliochukuliwa na chama chake, umefanyika
mapema.
Mghwira ameyasema hayo leo Alhamisi katika Ofisi ya Mkoa wa Kilimanjaro mjini hapa, mara baada ya kutia saini kitabu cha wageni.
Hata hivyo, RC huyo mpya amesema hatua hiyo itampunguzia mzigo na
kumrahisishia kazi tofauti na angeendelea kutumikia uenyeketi wa chama
huku akiwa mkuu wa mkoa kwa wakati mmoja.
"Mimi siyo mpinzani wa maendeleo nimepewa jukumu la kutekeleza maendeleo ya nchi," amesema Mghawira.
Mghwira ameongeza kuwa kwa nafasi aliyopewa atafanya kazi kwa kufuata Ilani ya CCM aliyopewa na Rais John Magufuli.

Post a Comment