Conte amtimua Costa Chelsea kwa njia ya meseji ya simu.
Conte amtimua Costa Chelsea kwa njia ya meseji ya simu.
Ndoto za Costa kubaki kwenye ulimwengu wa Stamford Bride zimezimwa kutokana na kauli ya kocha ambaye hivi sasa yupo kwenye harakati za usajili kwa
ajili ya kukisuka kikosi chake.
Taarifa za mchezaji huyo kuondoka kwenye klabu hiyo mabingwa wa England
msimu ulioisha, ziliaanza kuripotiwa kwenye vyombo vya habari kabla hata
ligi hiyo kumalizika.
Costa alikuwa anahusishwa kuhamia Ligi Kuu ya China hata hivyo hivi
karibuni alibadili mawazo na kutanga kwamba angependa kuendelea kubaki
England.
Nafasi yake kubaki Chelsea imekuwa ndoto kutokana na uongozi huo kuongeza kasi kumsajili mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku.
Mchezaji huyo mwenye miaka 28 amepewa taarifa za kutokuwapo kwenye mipango ya Conte jambo lililomfanya kuiwa njiapanda.
“Nimetumiwa ujumbe mfupi kwenye simu kutoka kwa Conte akisema sipo
kwenye hesabu zake za msimu ujao” alisema Costa alipokuwa akizungumza na
waaandishi wa habari wakati timu yake ya Hispania ilipotoka sare ya
mabao 2-2 dhidi ya Colombia jana Jumatano.
Costa alisema huenda kocha wake amechukua uamuzi huo kutokana na kufanyua vibaya msimu uliopita.

Post a Comment