Mwambusi ameitetea klabu ya yanga baada ya kutolewa kwenye michuano ya SportPesa Cup.
Mwambusi ameitetea klabu ya yanga baada ya kutolewa kwenye michuano ya SportPesa Cup.

Mwambusi ambaye kwenye michuano ya Supersport Super Cup amechukua
nafasi ya Kocha mkuu Lwandamina ambae yupo likizo amesema klabu ya Yanga
imetolewa kwa kukosa muda wa maandalizi kwani michuano hiyo haikuwa na
muda mrefu wa kuruhusu vilabu kujiandaa.
“Tumetolewa kweli michuano ilikuwa ni migumu kwetu hatukuwa na muda wa
kutosha wa maandalizi ya michuano hii muda ulikuwa mfupi sana, hii
imetuathiri sana kwenye michezo yetu yote miwili”Amesema Mwambusi mapema
baada ya mchezo kumalizika.
Klabu ya Yanga inakuwa timu ya nne kutolewa kwenye michuano hiyo yenye
msisimko wa aina yake inayodhaminiwa na kampuni ya Kubashiri ya
SportPesa, baada ya Simba,Singinda United na Jang’ombe Boys ya Zanzibar.
Post a Comment