Maamuzi ya Bunge kuwafungia Wabunge kuhudhuria vikao ni ukiukwaji wa KATIBA.
Maamuzi ya Bunge kuwafungia Wabunge kuhudhuria vikao ni ukiukwaji wa KATIBA.

Haki ya wabunge kuhudhuria vikao na kuwawakilisha wananchi wa majimbo
yao ni ya kikatiba na kanuni feki za Bunge zinazolipa Bunge mamlaka ya
kuwasimamisha wabunge kutekeleza majukumu yao ya kikatiba zinakiuka
katiba ambayo wabunge hawa waliapa kuilinda na kuitetea Katiba husika!
Bunge halipo juu ya katiba na ndiyo maana wabunge wote huapa kabla ya
kuanza shughuli za Bunge ya kuwa wataitii katiba ambayo hakuna mahali
ndani ya katiba hiyo wamepewa mamlaka ya kuwasimamisha wabunge na
kuwapora wananchi wanaowawakilisha haki yao ya kikatiba ya uwakilishi.
Tusipokuwa waangalifu itafikia wakati Bunge linamsimamisha Mbunge kwa
miaka mitano na kuwapora wananchi wa jimbo husika haki yao ya kikatiba
ya kuwakilishwa kwa kipindi chote cha uwakilishi.
Adhabu za kikanuni za Bunge hazina mamlaka ya kupora wananchi haki zao za kikatiba kama kuwakilishwa.
Kama Mbunge kavunja kanuni Bunge linaweza kumpa faini ili aathirike
Mbunge mwenyewe bila kuathiri haki ya kuwakilishwa ya wananchi wa jimbo
lake.
Spika Job Ndugai kuwaadhibu askari walioheshimu haki za binadamu pia
linatia aibu si kwake tu bali kwa Bunge zima na taifa kwa ujumla.
Chanzo JF
Post a Comment