click here

click here

Jaji Francis Mutungi ambaye ni msajili wa vyama vya siasa amezungumzia sakata la Maalim Seif Kufungua ofisi mpya za CUF.

Jaji Francis Mutungi ambaye ni  msajili wa vyama vya siasa amezungumzia sakata la Maalim Seif Kufungua ofisi mpya za CUF.

Chama cha Wananchi (CUF) kimefungua ofisi mpya  katika eneo la Mtaa wa Idrisa Kata ya 
Mzimuni, Magomeni wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam
Akizungumzia sakata ilo msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi, alisema hajapokea  taarifa yoyote ya chama hicho, kufungua ofisi mpya zaidi ya kuona katika vyombo vya habari.
“Ukiondoa taarifa za kwenye media sijapata taarifa yoyote kutoka CUF labda wawe wameleta leo, lakini naamini chochote wanachofanya wanaelewa taratibu wataleta taarifa, “ alisema Jaji Mutungi.
Jaji Mutungi alisema sheria inawataka wanapofungua ofisi watoe taarifa ndani ya siku 14, ambazo hazijaisha hivyo anaamini wanajua hilo. 
  Nae katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa wamefungua ofisi hizo, baada ya tukio la kuvamiwa katika Ofisi Kuu  zilizopo maeneo ya Buguruni na kundi la Profesa Ibrahim Lipumba.
Jaji Mutungi alisema atakapopokea taarifa rasmi ataangalia kama taratibu zilifuatwa kwani ufunguaji wa ofisi mpya una taratibu zake. 
“Nikiletewa taarifa ndio nitajua kama walifata taratibu au la, ufunguaji wa ofisi una taratibu zake najua wanazijua pia, “ alisema Jaji Mutungi.
Alisema taarifa hiyo ataipata kutoka kwa mwenyekiti au msemaji wa chama, ambaye ni katibu mkuu ambao wanatambuliwa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa. 
Akizindua ofisi hiyo  Maalim Seif alisema ofisi hiyo imetolewa na wabunge 40 wa CUF.
alieleza kuwa uamuzi wa wabunge hao kumpatia ofisi ya kufanyia kazi hapo ni kitendo cha kiungwana na kiungwe mkono na wanachama wote. 
  Seif aliendelea kusema kuwa kwa miezi 10 sasa, wamekuwa wakishindwa kufanya kazi kwa upande wa Tanzania Bara, jambo ambalo limewaathiri hivyo kupatiwa ofisi kutamsaidia kutimiza majukumu bila hofu yoyote.
Katibu huyo alisema ana imani na mahakama kuwa itawapatia haki stahiki hivyo kuwataka wanachama kuendelea kuwa na subira.

No comments

Powered by Blogger.