Ajib adai bila Milioni 60 hatosaini Singida United
Ajib adai bila Milioni 60 hatosaini Singida United
Ibrahim Ajib ambaye ni kiungo mshambuliaji wa Simba, amewataka Singida United
kumpa milioni 60 ili wapate saini yake kwa ajili ya kuwatumikia msimu
ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Ajib ambaye kaonyesha nia ya kuachana na Simba baada ya mkataba wake kuisha
na kwenda kutafuta changamoto nyingine ya soka, jina lake limetajwa na
kocha wa Singida United, Hans Pluijm kwenye kikosi chake.
Tayari Ajib amekwishaweka bayana kuwa anahitaji fedha hizo na
endapo itashindikana kupatiwa pesa hizo, hawezi kujiunga na timu hiyo mpya kwenye Ligi Kuu
msimu ujao.
Mbali na Ajib pia timu hiyo imeonyesha nia ya kumtaka mchezaji wa Yanga, Deus Kaseke ambaye naye anahitaji Sh milioni 40.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Singida United, Festo Sanga,
alithibitisha kufanya mazungumzo na wachezaji hao, lakini bado
hawajafikia hatua ya kuwafanya wasaini katika klabu hiyo.
“Ni kweli tunawahitaji na tumefanya nao mazungumzo na tumeweka wazi
kiasi ambacho tunacho mkononi, ila inaonekana wao bado hawapo tayari,
hivyo tunawasubiri wao wakiwa tayari sisi hatuna shida muda wowote
wakitufuata tutasaini,” alisema Sanga.
Alisema kuwa malengo yao msimu huu ni kusajili wachezaji 25, wapya
wakiwa 14, saba kutoka nje na saba wengine kutoka ndani, huku mpaka sasa
wachezaji wa ndani bado watatu kwa kuwa wamesajili wawili tu.
Post a Comment