Lissu afunguka kuhusu sakata la Mchanga wa Madini
Lissu afunguka kuhusu sakata la Mchanga wa Madini
Tundu Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki, kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),amesema kuwa msimamo wake wa
kupinga kitendo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John
Magufuli cha kuzuia mchanga wa dhahabu kusafirishwa nje uko pale pale.
Lissu amesema hayo alipokuwa bungeni mjini Dodoma, aliongeza kwa kusema kwamba kuzuia mchanga
huo wa dhahabu kusafirishwa kwenda nchi za nje kutaathiri uchumi kwani
atakuwa ameenda kinyume na mikataba ya kimataifa.
“Rais Dkt. Magufuli amefanya kitendo ambacho ni kinyume na mikataba ya
kimataifa, kwa hiyo hapa tutegemee hasara kubwa na kutengwa na jumuiya
ya kimataifa,”amesema Lissu

Post a Comment