Washambuliaji 2 wa London watajwa na polisi
Washambuliaji 2 wa London watajwa na polisi
Na BBC
Polisi nchini
Uingereza imewataja wanaume wawili kati ya watatu waliofanya shambulio
katika mji wa London Bridge siku ya Jumamosi na kuwauwa watu saba kabla ya
kuuawa kwa risasi .
Mmoja wao alikuwa Khuram Butt, alikuwa akitambuliwa na huduma za usalama za Uingereza.Aliwahi kuonekana kwenye kipindi cha Televisheni mwaka jana kilichoangazia kundi lenye itikadi kali linalounga mkono Islamic state .
Wote waliokuwa wamekamatwa na polisi kufuatia mauaji hayo wameachiliwa bila mashtaka yoyote.

Post a Comment