TSJ Haikamatiki Kwa Wanahabari bora.
TSJ Haikamatiki Kwa Wanahabari bora.
Na Nyamarasa Mgaya
Bila shaka watu wengi wasomi na ambao hawajasoma wanaelewa
kuwa Elimu ndiyo urithi pekee na bora kwa kila Mtu kuupata ili umsaidie
katika maisha ya baadae.
Elimu imezungumzwa na watu tofauti katika jamii, wazazi, viongozi na hata vitabu vitakatifu kwa lengo la kuonesha umuhimu wake.
Kumbe chanzo cha ufahamu wa mtu huanzia katika elimu na
kuonekana katika jamii namna mtu huyo anavyofikiria na hata kimawazo na
ushauri.
"Kila Mtu anataka kufanikiwa lakini si kila Mtu yupo
tayari kushika majukumu na wajibu wa kumpeleka kwenye mafanikio" alisema
mwl Nyerere.
Japo wengi huweka malengo ya kusoma sana na kupata elimu bora lakini hushindwa kutokana na kutokubali majukumu na wajibu wao.
Mara nyingi kushindwa kutimiza malengo ya Mtu hutokana na
kutofanya uchaguzi sahihi wa sehemu bora itakayosaidia kutimiza
mafanikio yake.
Uwepo wa Elimu bora Nchini ni matokeo chanya kwa Taifa kuwa
na wasomi wenye fikra, mawazo, ujuzi na ushauri utakaowezesha kusonga
kwa maendeleo hapa nchini.
Serikali yetu imekuwa ikilalamikia uwepo vyeti feki na
watumishi hewa, kwa asilimia kubwa wengi wao walipata elimu isiyo bora
na wengine kusoma katika sehemu ambazo hazina sifa.
Suala hili linarudisha nyuma maendeleo ya Taifa na kwa Mtu binafsi, kuwa msomi bora kunaanza na sehemu utakapoita elimu hiyo.
Kutokana na harakati za kufanya uchaguzi wa sehemu bora
itakayosaidia kutimiza lengo lako, tukabisha hodi katika chuo cha
uandishi wa habari cha Tsj.
Chuo hiki ni moja kati ya vyuo vikongwe katika ufundishaji wa taaluma ya uandishi wa habari na utangazaji hapa nchini.
Time school of journalism (TSJ) kilianzishwa rasmi mei 15
mwaka 2000 katika eneo la msimbazi center kikisimamiwa na watu binafsi
walioungana na kuanzisha kama taasis iliyoitwa "time" (Tanzania
institute of media education).
Tangu kuanzishwa kwake kimekuwa kikikabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo za kifedha na majengo lakini bado kimeendelea kudumu
na kuwa moja kati chuo chenye sifa kubwa.
Taarifa zilizotolewa na mkuu wa Chuo Bi Suzana Lucas
zinaeleza kuwa katika vituo vingi vya Habari hapa nchini vina
wafanyakazi waliosoma Tsj.
Bi Suzana aliongeza kuwa chuo hicho kimeweza kutoa
waandishi wengi wa habari hapa nchini na kimataifa, Salim kikeke
mtangazaji wa BBC akiwa ni mmoja wa wanafunzi wa Tsj.
Kufanikiwa kwa mtu ama taasis hukamilika pale anapojiwekea
malengo na kuyasimamia ipasavyo ili yatimize mafanikio aliyokua akiwaza
namna ya kuyatimiza.
Pia Tsj ilipoanza ilikuwa na malengo mazuri ambayo yamefanya kudumu katika ushindani wa vyuo vingi vya Habari nchini.
Mkuu wa Chuo cha Tsj Bi Suzana Lucas alieleza kuwa shauku
yao ni kutoa wanahabari bora watakaoweza kufanya kazi zao kwa kujiamini
kwa kufuata taaluma walioipata.
Chuo hiki kipo cha ya wakurugenzi ambao majini yao
tumeyahifadhi na wanasimamia na kuhakikisha shughuli za ufundishaji na
mambo mengine yanaendelea kama kawaida.
Tsj ni moja kati ya vyuo vya Habari vinavyoamiwa hapa
nchini katika kutoa mafunzo ya uandishi bora wa habari na utangazaji
kitaifa na kimataifa.
Huenda msomaji unaesoma makala hii ulikuwa ukiwaza ni chuo
gani unaweza ukasomea ama akamuelekeza ndugu yako na hata rafiki yako
ili akasomee taaluma ya habari bila shaka umepata jibu sahihi
Ili Taifa lisonge mbele kimaendeleo lazima lipate waandishi
bora wa habari watakaoweza kuibua mambo yaliyojificha katika jamii na
taasis mbalimbali za umma.
Kutokana na tamko la serikali kupitia waziri wa Habari,
utamaduni, sanaa na michezo mh Harrison mwakyembe kuomba wanahabari
kusoma na kuhakikisha japo mwandishi wa habari kuwa na Elimu ya stahada,
Tsj inawakaribisha wanahabari kujiunga na chuo hicho.
Chuo cha Tsj kwa sasa kinasajili wanafunzi mia 3 kila mwaka
ikiwa ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na wanafunzi 6 kilichoanza nao
mwaka 2000.
Pia kina mpango wa kujenga majengo yake binafsi katika eneo
la Bunju jijini Dar es salaam na kuachana na upangaji katika majengo ya
watu binafsi.
Chuo cha Tsj kinapatika katika eneo la Ilala bungoni jijini
Dar es salaam na kinatoa taaluma ya uandishi wa habari kwa ngazi ya
astahada na stahada pekee.
Ili uwe na Elimu bora itakayosaidia kutimiza malengo yako
lazima utafute chuo bora kitakachosaidia kumiza ndoto yako, maamuzi yako
ya Leo ndiyo mafanikio yako ya kesho.

Post a Comment