STORYGRAM1:Gazeti la Mawio lafungukiwa kwa miaka miwili kwa kosa la kuchapisha Habari kuhusu JK na Mkapa kuhusika na ufisadi wa Madini.
Gazeti la Mawio lafungukiwa kwa miaka miwili kwa kosa la kuchapisha Habari kuhusu JK na Mkapa kuhusika na ufisadi wa Madini.

Serikali kupitia Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk
Harrison Mwakyembe imelifungia gazeti la Mawio kuchapishwa kwa miezi 24
kuanzia June 15.
Taarifa iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (Maelezo), Dk Hassan Abbas imesema waziri amechukua
hatua hiyo kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 59 cha Sheria
ya Huduma za Habari namba 12 ya mwaka 2016.
Amesema hatua hiyo inatokana na gazeti hilo katika toleo namba 196 la
15-21 Juni, 2017 kuchapisha katika ukurasa wa mbele picha za marais
wastaafu Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete ikiwahusisha na sakata la
mchanga wa madini.
Pia, katika ukurasa wa 12 wa gazeti hilo limechapisha makala
iliyoandikwa Lissu: Mkapa, Kikwete wataponaje? Kuwatuhumu viongozi hao
kuhusika katika sakata la madini wakati ukweli ni kwamba hawakuwa sehemu
ya uchunguzi wa kamati za Rais John Magufuli na wala matokeo ya kamati
hizo hayakuwatuhumu kwa kosa lolote.
Taarifa ya Waziri Mwakyembe kwa mhariri mkuu wa gazeti hilo imesisitiza
kuwa, licha ya utetezi wao, habari hizo si tu zimekiuka agizo la
Serikali lakini pia, zimekiuka vifungu vya 50(a), (b), (c), (d) na (e)
vinavyokataza uandishi wenye dhamira hasi.
“Sina budi kulifungia gazeti lako na kukutaka usitishe kulichapisha kwa
nakala ngumu au ya mtandaoni kwa kipindi cha muda wa miezi ishirini na
nne 24 tangu tarehe ya barua hii kwa mamlaka niliyopewa chini ya sheria
ya huduma za habari namba 12 ya mwaka 2016 kifungu 59,” imesema taarifa
ya Dk Mwakyembe kwenda kwa mhariri wa Mawio.
Waziri pia amevipongeza vyombo vingi vya habari ambavyo amesema kuanzia
leo vimefuata weledi wa taaluma na misingi ya sheria, vikitii agizo la
Serikali kwa kutowaingiza katika sakata hilo pasipo hoja za msingi
viongozi wastaafu.
Post a Comment