click here

click here

STORYGRAM1: MAAJABU: WEZI WAVAMIA NA KUPIKA KUKU, KULA NA KUOSHA VYOMBO KISHA KUIBA NA KUTOKOMEA KUSIKOJULIKANA.


  MAAJABU: WEZI WAVAMIA NA KUPIKA KUKU, KULA NA KUOSHA VYOMBO KISHA KUIBA NA KUTOKOMEA KUSIKOJULIKANA.

Kenya Majambazi wamevamia nyumba ya Mchungaji eneo la Mweiga katika Kaunti ya Nyeri wakachinja kuku wake, wakampika na kumla na kisha wakaosha na vyombo walivyotumia.

Mchungaji Joseph Muraya alisema kuwa wezi hao waliingia katika eneo lake majira ya saa mbili usiku  na kuwatisha kuwaua kwa kuwapiga risasi endapo wangewataarifa majirani zao.

Nilirudi nyumbani  majira ya saa mbili na nilishangaa kukuta geti langu limefunguliwa nusu, nilisikia mbwa wana bweka na nilipokwenda kuwaangalia nilikuta mtu mmoja yupo nje, na baadae niligundua kuwa kuna wengine watano wamo ndani, alisema mchungaji huyo.

Majambazi hao baada ya kupika na kuosha vyombo, waliondoka na mali  ambazo thamani yake haijulikani.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Nyeri, Peter Okiring alisema kuwa Jeshi la Polisi tayari limeanza uchunguzi kuwabaini wahalifu hao.

No comments

Powered by Blogger.