click here

click here

Shamsa Ford Amuoneaa Wivu Odama

Shamsa Ford Amuoneaa Wivu Odama

  Na Rahma Kigua
Mwanadada anayefanya vizuri kwenye tasnia ya filamu Nchini, Shamsa Ford amefunguka juu ya kuonea wivu mahusiano ya muigizaji mwenzake, Jenipher Kyaka 'Odama' kwa kuyafanya kuwa na usiri mkubwa huku akipongeza na kusema ndivyo inavyopaswa mtoto wa kike kufanya kwenye mapenzi.

Shamsa amesema hayo alipotoa maoni yake katika ukurasa wa instagram wa Odama na kufunguka kuwa  anapenda jinsi muigizaji huyo anavyoweza kuweka mahusiano yake ya mapenzi kuwa faragha yake peke yake na kuongeza kuwa anatamani kama siku zingerudi nyuma asingethubutu kumuonyesha mpenzi wake hadharani bali mume wake wa ndoa.

"Napenda unavyoweka mahusiano yako ya mapenzi 'private'. Sijawahi ona hata siku moja umempost sijui boyfriend na hicho ndo kitu kizuri kwa mtoto wa kike. Mimi kwa upande wangu ningerudisha siku nyuma kipindi kile nipo single nisingempost au kumuweka wazi mwanaume yoyote niliyekuwa naye kipindi kile kwenye mahusiano. Natamani mume wangu ndio angekuwa mwanaume wa kwanza kwa watanzania kumjua" - Shamsa Ford alifunguka.

No comments

Powered by Blogger.