Msechu ametangaza dau la milioni moja kwa mtu akayemuandikia wimbo mzuri.
Msechu ametangaza dau la milioni moja kwa mtu akayemuandikia wimbo mzuri.

Mwimbaji huyo amesema kuwa mtu yeyote mwenye wimbo mkali amtafute na
wakae chini kuongea kwa ajili ya kupatana bei, lakini kiasi cha fedha
unachoweza kupata kinaweza kufika hadi sh. milioni moja.
“Kuna mtu amenicharge juzi wimbo mmoja sh. milioni moja na ni wimbo
mkubwa sana, ninafikiri ndio wimbo utakaofuata baada ya Ramadhan,”
Msechu amekiambia kipindi cha Ladha 3600 cha E Fm.
“Kuna mdada mmoja anakaa Arusha ameniandikia nyimbo mbili aiseee!!,
nilitengemea hata atanidai milioni tano au sita lakini alikataa kabisa
akaniambia kwa heshima yako wewe ziimbe tu, unaona kabisa wapo watu
wenye vipaji hivyo lakini wamejificha,” ameongeza.
Msechu ameongeza kuwa toka awali alishaweka wazi kuwa yeye hajui
kuandika nyimbo hivyo watu wasishangae kwani anafanya hivyo ili kuepuka
kukurupuka kutoa nyimbo kama ilivyokuwa awali ila sasa hivi anajaribu
kujipa muda.
Post a Comment