MOON JAE IN, RAIS MPYA WA KOREA KUSINI, MWENYE MALENGO MAZURI NA KIM JONG UN
MOON JAE IN, RAIS
MPYA WA KOREA KUSINI, MWENYE MALENGO MAZURI NA
KIM JONG UN
Na Erick Paschal,TSJ
erickpaschalkavishe@gmail.com
Ni wiki kadhaa zimepita tangu Moon Jae in achaguliwe
kuwa Rais mpya wa Taifa la Korea Kusini, ameshinda kwa kishindo na kuwa Rais wa
12 wa Taifa hilo na kuziba pengo la aliyekuwa Rais wa taifa hilo Bibi Park Geun
hye, aliyejiuzulu kwa kushinikizwa na wananchi wa Korea kwa tuhuma za ufisadi toka
mwishoni mwa Januari,2017.
Rais
wa Korea Kusini Bwana Moon Jae In. (Picha kwa msaada wa mtandao wa Wikipedia)
Bwana
Moon ameonekana kuwa na mtazamo tofauti kuliko inavyotegemewa na raia wengi wa
Taifa hilo lililopo Barani Asia. Kubwa alilolinadi Rais huyu mpya, ni
kuimarisha kwa mara nyingine uhusiano wake na Korea Kaskazini, Taifa ambalo
limekuwa na mgogoro wa muda mrefu na Taifa hilo. Kitu kilicho kinyume na sera
za taifa hilo kwa muda mrefu. Bwana Moon anataka kupunguza na ikiwezekana
kuondoa kabisa uhasama uliopo kati ya Korea kusini na Korea Kaskazini.
Lakini si jambo hilo tu linaloishtua Dunia
kwa sasa, kwani mara baada ya kuapishwa Bwana Moon, amehoji mfumo wa ulinzi wa
Marekani na kuhoji ni kwanini Marekani iliweka makombora ya Ulinzi katika ardhi
ya nchi yake. Kitu ambacho wengi wao hawakukitegemea kwani Marekani na Korea
Kusini wamekuwa washirika wakubwa tena wakiwa bega kwa bega kupingana na Korea Kaskazini.
Ambayo imekuwa ikirusha makombora ovyo kwa nchi jirani kama vile Japan pamoja na
Korea kusini. Rais Moon Amekaririwa na Vyombo vya Habari mbalimbali akisema
atapenda kuitembelea Pyongyang katika hali nzuri.
Hatahivyo
Rais Moon amesema atashughulika sana kuliunganisha Taifa hilo linalokabiliwa na
ufisadi ambao ulisababisha mtangulizi wake kushitakiwa, mbali na kulipa
kipaumbele swala la kuimarisha Uchumi wa Taifa hilo.
Pia Bwana Moon ana mpango wa kutenga zaidi ya dola
billion 8.9 kuinua ajira katika taifa hilo, malengo yake ni kuanzisha ajira
zaidi ya laki nane na kumi kwa vijana wa Korea kusini.
Lakini
raia wengi wa nchi hiyo wameonekana kuwa na wasiwasi na Kiongozi huyu mpya, juu
ya kuungana na Korea Kaskazini kwani wananchi wa Korea Kusini wanahisi kuna
uwezekano wa vita kujirudia tena katika harakati za kuungana. Kwa upande wa
vijana ambao wengi wao ni wasomi wa elimu ya juu, wanaona suala hili linaweza
kuliingiza rasmi vitani nchi hiyo na jirani yake Korea Kaskazini.
TUTAZAME
MAISHA
YAKE BINAFSI
Ana
umri wa miaka 64, amezaliwa Januari 24 mwaka 1953 katika eneo la Geoje, ni
mtoto wa kwanza kwenye uzao wa baba yake ajulikanaye kwa jina la Moon Yong-hyung
na mama yake Kang Han-ok. Baba yake alikuwa ni mkimbizi kutoka Kusini mwa
Hamgyeong province ambalo kwa sasa ni eneo la Korea ya Kaskazini, ana mke mmoja
afahamikaye kwa jina la Kim Jung-sook, na ni baba wa watoto wawili.
Kitaaluma
ni Mwanasheria, pia ni mwanaharakati wa haki za binadamu. Amewahi kufaulu elimu
ya juu zaidi kuhusiana na masuala ya sharia, lakini hakuweza kupandishwa cheo
na kuwa jaji wa mahakama au Mwendesha mashitka wa Serikali kutokana na harakati
zake za haki za kibinadamu alizozifanya,
ili kupingana na udikteta wakati akiwa ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha
Kyung Hee. Ndipo akaamua kubaki kama wakili au mwanasheria, pia amehudumu kwa
nafasi mbalimbali katika taifa hilo. Amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Ikulu kipindi
cha Raisi Roh Moo-hyun machi 2007 mpaka Februari 2008, Rais Moon pamoja na Rais
Roh, kimahusiano walikuwa ni marafiki. Bw. Moon alikuwa mtu wa karibu na Rais
huyo kabla ya Rais huyo wa zamani wa Korea Kusini kujiua mwenyewe Mei 23 mwaka
2009 akiwa na umri wa miaka 62.
Rais Moon
Jae-in ni muumini mzuri wa dhehebu la kikatoliki na kiongozi wa pili kutoka
katika Dini ya kikristo ukiachana na Rais mstaafu Kim Dae-jung.
Post a Comment