click here

click here

Majeshi ya serikali ya Syria yaukomboa mji wa mashariki ya Aleppo

 Wanajeshi wa Syria leo wameukomboa mji wa Mashariki ya jimbo la Aleppoambao ni muhimu kwa wapiganaji wanaojiita Dola la Kiislamu IS.


Taarifa za kijeshi zinasema vikosi vya serikali ya Syria vinakaribia kutimiza lengo lake la kuwafukuza wapiganaji hao wa Jihadi kutoka eneo hilo.
 
Operesheni ya kijeshi inayosimamiwa na vikosi vya Urusi ambayo ilianza katikati ya mwezi Januari kwa sehemu kubwa imewezesha kukombolewa kwa eneo la Maskana, lililo Magharibi mwa ukingo wa ziwa Assad katika jimbo la Aleppo.

RamiAbdelrahman mkurugenzi wa shirika linalofuatilia haki za binadamu Nchini Syria amesema jeshi la Syria limekomboa zaidi ya miji na vijiji 200 tangu lilipoanzisha operesheni yake Mashariki ya jimbo la Aleppo. Zaidi ya watu 320,000 wameuawa katika vita vya Syria vilivyoanza kwa maandamano ya kuipinga serikali mnamo mwezi Machi mwaka 2011.
                                                              
                                                                         Na: Dw swahili

No comments

Powered by Blogger.