click here

click here

JIFUNZE JINSI YA KULIMA TIKITIMAJI

JIFUNZE JINSI YA KULIMA TIKITIMAJI

Na. Monica Haruna

   Tikitimaji ni zao lenye Maji mengi na linalotumia Siku 65-90 kutoka kupadwa hadi kuvunwa kulingana na aina ya mbegu itakayokuwa imetumika kupanda shambani. Kuna maeneo mengine yana joto ambayo tikitimaji linaweza kukomaa na kupata afya nzuri mfano wa maeneo ya Pwani, tikitimaji linaweza kukuwa kwa ubora zaidi, na mazao mengine hukomaa mapema ukilinganisha na maeneo ya milimani yenye baridi, kwa hiyo maeneo ya milimani hayaruhusiwi kwa kilimo cha matikitimaji.

   Hivyo basi kama unataka kulima zao la tikitimaji, tafuta sehemu zenye hali ya hewa nzuri kuendana na mahitaji yako.
   Chagua eneo ambalo halina hisitoria ya kuwa na magojwa au wadudu wanaoshambulia tikitimaji. Na eneo ambalo Lina Maji mengi ya kumwagilizia hili usiwe na usumbufu wa kumwagilia.
   Ni  bora sana na ni vizuri ukijua eneo lenye udongo mzuri  was kulimia tikitimaji, tikitimaji linasitawi sana katika udongo wa tifutifu na kichanga lakini udongo wa mfinyanzi sio mzuri sana kwa kulimia zao la tikitimaji kwani husababisha matunda kualibika (kuwa na nyufa).

Kuandaa shamba
 Unapotaka kulima andaa shamba lako zuri na unatakiwa use umeandaa matuta yenye upana wa mita 2 na urefu was sentimenta 30 ili kusaidia mizizi na ya tikitimaji hili kuzuia Maji kutuama hasa katika kipindi cha mvua.
   Kipindi cha ukuaji tikitimaji linatakiwa unyevunyevu wa  udongo wakati wote lakini maji yakizidi wakati wowote utapelekea tikitimaji kupasuka na kupunguza ubora wa matunda

 Upandaji
Tikitimaji upandwa kati ya mita 1-2 kati ya mmea na mmea, na uwekwa sentimenta 2-5 kwenda chini (shimo la kupandia) na kati ya mstari na mstari iwe mita 2 kila Shimo.

Utunzaji wa mimea
Mbolea ya samadi inatakiwa kwa kiasi cha 4-6 tani kwa ekari na udongo wiki 1 kabla ya kupanda, na kama hakuna mbolea ya samadi unaweza kutumia yaramila winner au DAP unalazimika kuweka kipimo cha gram 5 kwa kila shimo na huakikishe mbolea na mbegu havigusani baada ya niche kutokea.

Umwagiliaji
Kumwagilia zao la tikitimaji au mazao yote ni kuhimu sana. Lakini unapokuwa unamwagilia Maji machache kipindi cha kupanda husababisha kutoota kwa mbegu nakipindi cha kuweka Maua husababisha matunda machache kutokeza na matunda kukosa maumbo yake.

Kupalilia shamba
Illi kupata matunda mazuri, in vyema kupunguza mmea urefu pale unapoona mmea umefikia urefu wa kutosha ili kusaidia kitenganisha matawi ya pembeni ambayo Mara nyingi ndiyo ubeba Maua ya kike.
Hunatakiwa kusafisha shamba lako likiwa tayari na magugu, pia magugu husababisha baadhi ya magojwa katika mmea wako.
Pale matunda yanapokuwa mengi yanatakiwa kupunguzwa hili yabaki machache na kupata hewa vizuri.

MAGOJWA YANAYOSHAMBULIA TIKITIMAJI
Yapo magonjwa mengi yanayoshambulia tikitimaji hususan usipotumia dawa za kuua au kusaidia kukuza mimea, magonjwa hayo ni kama vile:
Ubwiru
Dalili zake
Majani huwa yakijani kuwa kama yanakauka na madoadoa meusi kwa umbali
Tiba yake
Dawa zenye viambato vya metalaxy na mancozeb,
Kata kiuno
Ugojwa huu husumbua sana miche midogo, huanzia aridhini husababisha miche midogo kuanguka chini maana ula sehemu ya shina.
Tiba yake
Tumia ridomil gold na anza kupulizia Mara tu baada ya mimea yako kuota.

No comments

Powered by Blogger.