Islamic State wavamia Bunge na Kuwamiminia Risasi Wabunge Nchini Iran.
Islamic State wavamia Bunge na Kuwamiminia Risasi Wabunge Nchini Iran.

Kundi la kigaidi lijulikanalo kama Islamic State (IS) limevamia na kushambulia
bunge la Iran pamoja na jengo la kaburi la kiongozi wa kidini wa nchi
hiyo, Ayatollah Khomeini linalojulikana kama Mausoleum katika mji mkuu
wa Tehran ambapo watu 12 wameuawa na wengine kujeruhiwa.
Mashambulizi hayo yamefanyika leo kwa wakati mmoja. Vyombo vya dola vya
ilani vimeeleza kuwa washambuliaji watano wenye silaha waliingia ndani
ya jengo la bunge, na mmoja alijitoa mhanga kwa kujilipua kwa bomu.
Aidha, ripoti zimeeleza kuwa magaidi waliingia ndani ya bunge hilo
kupitia mlango wa raia wakiwa wamevalia mavazi ya kike.
Hata hivyo, wanausalama walifanikiwa kuzima mashambulizi hayo baada ya
saa kadhaa za kusikika milio ya risasi. Kituo cha runinga cha Iran
kimeripoti kuwa washambuliaji wote waliuawa na wanausalama.
Magaidi wa IS wametoa tamko kukiri kutekeleza shambulizi hilo likiwa ni
shambulizi la kwanza ndani ya Iran na kutishia kuwa wataendelea
kutekeleza mashambulizi mengine wakilenga waumini wa Shia ambao ni
wengi.
Rais wa Iran, Hassan Rouhani amesema kuwa ugaidi ni tatizo la dunia
nzima na kutoa wito kwa mataifa yote kushirikiana kuendesha vita dhidi
ya ugaidi.
Iran imekanusha kuwepo kwa utekaji au kushikiliwa kwa watu ndani ya jengo la bunge wakati wa mashambulizi hayo.
Post a Comment