Bajeti Mpya: Wafanyakazi Tumeikosea Nini Awamu ya Tano ?
Bajeti mpya: wafanyakazi tumeikosea nini awamu ya tano ?
Nimesoma hotuba ya bajeti kurasa zote kuanzia ukurasa wa kwanza mpaka wa
mwisho hakuna chochote kilichozungumzwa kuhusu maslahi ya mfanyakazi wa
umma hususani mshahara wa mtendaji huyu wa serikali.
Licha ya matambo na mbwembwe nyingi katika uwasilishaji lakini serikali
imeshindwa hata kutaja kima cha chini tu cha mshahara!Imeshindwa hata
kusema tu maneno machache ''tumezingatia maslahi ya mtumishi katika
bajeti hii''
Hii serikali toka iingie madarakani imekuwa na mazoezi kandamizi tu kwa
mfanyakazi, watumishi hewa, vyeti feki, lawama za kila aina lakini
imekuwa jeuri kuhusu kuzingatia maslahi ya wafanyakazi hawa.
Wabunge tunawaomba msimamie na kupigia kelele suala hili katika mjadala wa bajeti.
Chanzo JF

Post a Comment